Home » » UMEME WA ZOLA WAINGIA TANGA, YAFUNGUA DUKA MTAA WA MARKET STREET MJINI TANGA

UMEME WA ZOLA WAINGIA TANGA, YAFUNGUA DUKA MTAA WA MARKET STREET MJINI TANGA



Tangakumekuchablog
Tanga, MWENYEKITI wa mtaa wa Centrol Tanga, Diana Mussa, amewataka wakazi wa eneo hilo kuweka mazingira ya usafi kwa kila nyumba ili kuondosha kitisho cha magonjwa ya miripuko na kusema  kuwa  ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa duka la kuuza umeme la  Zola lililopo barabara ya Markert Street Tanga juzi , Diana amesema agizo hilo litakuwa endelevu na ofisi yake ikiongozwa na yeye kila siku asubuhi atafanya ukaguzi kwa kila mtaa.
Amesema halmashauri ya jiji imeweka vyombo maalumu vya kuhifadhia takataka na magari ya kusomba taka mtaani hivyo kutaka kila mmoja kuhakikisha eneo lake linakuwa katika mazingira mazuri.
Akizungumza kwenye ufunguzi huo,Meneja mauzo kanda ya Kaskazini Tanga na Kilimanjaro, Peter Laizer, amewataka wajasiriamali wadogowadogo  kutumia umeme wa Zola na kusema  kuwa ni wa gharama nafuu.
Amesema Wajasiriamali wa mbogamboga na matunda wanaweza kuinua kipato chao kwa kusindika na kuweza kusafirisha kwenda katika masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambako  watajitangaza tofauti na kutegemea mteja mmoja mmoja.
                                           
Amesema umeme huo ni mkombozi kwa watu wa kipato chote, cha chini, kati na juu na, umeme huo utaondolea adha mbalimbali kama za kuchaji simu mbali na nyumbani na ufuatiliaji wa taarifa katika Luninga pamoja na kusaidia watoto kusoma katika mwanga bora  nyakati za  usiku.
 “Umeme huu ni mkombozi kwa wananchi wa Tanga kwani ni rahisi, hauchukui muda kuupata na pia utawasaidia wananchi kuhifadhi kiasi cha pesa ambacho walikuwa wanakitumia kwa nishati nyingine kupata mwanga, Pia humsaidia mwananchi wa kipato cha chini kubadilisha maisha kwa kupata habari, taarifa pamoja na burudani, kwani mbali na taa na kuchaji simu pia utapata Radio na TV za sola”alisema Laizer
Alisema umeme huo  umekuwa mkombozi kwa wanafunzi wa vijijini ambao walikuwa hawana uwezo wa kujisomea usiku au husoma katika mwanga hafifu wa vibatari sasa wanapata mwanga  salama kwa afya ya mwili na macho.
                                                    Mwisho


 Mwenyekiti wa mtaa wa Centrol Tanga, Diana Mussa, katikati akikata uzi kuashiria ufunguzi wa dula la kuuza umeme wa Zola Markert Street mjini Tanga juzi , kushoto ni Msimamizi wa maduka ya Zola , Bethany Katen na kulia ni Mtendaji kata ya Centrol Bhati Marungu.
 Meneja Mauzo kanda ya Kaskazini maduka ya kuuza umeme wa Zola , Pitter Laizer akitoa maelezo ya matumizi wa umeme wa Zola wakati wa ufunguzi wa duka hilo juzi.


 Wakazi wa Tanga wakiangalia radio za kuchaji baada ya kuchajiwa kwa kutumia umeme wa Zola wakati wa ufunguzi wa duka la kuuzia umeme wa Mypower Tanga juzi
Habari hii ni kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa