KUFUATIA
Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na
wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa
madawati 100 kwa shule tatu.
Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga , Thobias Mwailapwa, Mkuu wa Idara Rasilimali
watu kiwabda cha Saruji , Diana Malambusi amesema msaada huo umekuja
baada ya kuona kero ya wanafunzi kusomea chini kutoisha.
Akizungumza
katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya, Thobias Mwailapwa,
amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement) na kuyataka mashirika na
taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya
wanafunzi kusomea chini.
Kwa
upande wake Afisa elimu shule ya msingi jiji , Khalifa Shemahonge,
amesema madawati hayo yatatumika kama inavyokusudiwa na kuahidi
kuyatunza ili kuongeza uelewa wa wanafunzi darasani.
Mkuu
wa Idara ya Rasilimali watu kiwanda cha Tanga Cement (Simba Cement),
Dianna Malambugi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, madawati 100 kwa shule tatu za msingi, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba za halmashauri ya jiji la Tanga kupunguza uhaba wa madawati na wanafunzi kusomea chini.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, akimkabidhi Afisa Elimu Shule ya Msingi halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa Shemahonge madawati 100 kwa shule tatu ya, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba yaliyotolewa na kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi kupunguza uhaba wa madawati kwa shule hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa mwenye suti bluu (katikati) na Afisa Elimu shule ya msingui halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa Shemahonge (kulia) wakiwa na wafanyakazi wa kiwanda cha Simba Cement mara baada ya makabidhiano ya madawati 100 kwa shule tatu za halmashauri ya jiji la Tanga . Walimu wa shule za msingi Magaoni, Kiruku, Martin Shamba na Mkombozi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga na wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement mara baada ya makabidhiano ya madawati 100 kwa shule hizo.
0 comments:
Post a Comment