Mkuu wa wilaya ya Handeni wa kwanzakushoto akisoma ramani ya mwaka
2007 akiwa na viongozi na wananchi ili kujua mpaka upo sehemu gani.DC Gondwe amefanikiwa
kusuluhisha mgogoro wa mpaka uliodumu kwa muda mrefu akiwa ameambatana
na Wakurugenzi wa halmashauri zote mbili uliohusisha Kijiji cha
Kweditilibe cha Handeni vijijini na kitongoji cha makinda kilichopo
Handeni Mji.
RAMANI YA 2007 ndiyo iliyotumika
kusuluhisha mgogoro huo ambapo aliwaeleza wananchi kuwa ramani hiyo
ndiyo iliyotumika kuweka mipaka ya maeneo husika Tanzania nzima na
hakuna mwenye mamalaka ya kuibadili isipokua Raisi mwenye mamalaka ya
Ardhi ya Tanzania nzima.
Mkuu wa wilaya Mh. Godwin Gondwe akisalimiana na mmoja wa wananchi wa
Wilaya ya Handeni kabla ya zoezi la kutatua mgogoro wa mpaka.
0 comments:
Post a Comment