Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akiongea na baadhi waandishi wa
habari mara baada mkutano ya
wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara
wa Sekta ya Mafuta nchini Dkt. Gideon Kaunda akiongea na baadhi waandishi wa
habari mara baada mkutano ya
wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini leo jijini Dar es salaam.
Picha na Ally Daud-
Maelezo
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
SERIKALI za Tanzania
na Uganda zinatarajia kuanzisha mradi wa uwekezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba
la mafuta unaolenga kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi hizo.
Mradi huo unatarajia kugharimu
kiasi cha Dola za Marekani bilioni nne na utekelezaji wake utaanza mwanzoni mwa
mwaka 2017.
Kauli hiyo imetolewa
leo Jumatatu (Machi 28, 2016) Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa alipokuwa na akiongea na waandishi wa
habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa sekta ya
mafuta nchini.
Prof. Ntalikwa amezitaja
fursa ambazo zitanufaisha taifa kuwa ni pamoja na kodi zitakazolipwa, kuongezeka
kwa wigo wa ajira kupitia miradi huo pamoja na tenda mbalimbali zitakazotolewa
wakati na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo.
“Tanzania ina kila sababu ya kupata mradi huo
kwa kuwa ina uzoefu wa kuwa na mabomba kama hayo manne nchini na tunajivunia
bandari yetu ya Tanga yenye kina kirefu kuliko bandari zote Afrika Mashariki”
alisema Prof. Ntalikwa.
Prof. Ntalikwa
amesema kuwa mwitikio wa wafanyabishara wa sekta ya mafuta nchini ni mzuri na
kubainisha kuwa wanatarajia kusafiri kuelekea nchini Uganda kujionea fursa
mbalimbali zinazopatikana nchini humo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini Dkt. Gideon Kaunda amesema
kwa upande wao wataitumia vyema fursa ya uwekezaji katika ujenzi wa mradi huo
na kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe
Magufuli.
0 comments:
Post a Comment