Home » » Samia: Kuna majipu ndani ya CCM.

Samia: Kuna majipu ndani ya CCM.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan,  amesema ndani ya CCM kuna watu majipu ambao wameficha makucha ili wasijulikane uovu wao. 
Samia alisema hayo juzi alipozungumza na viongozi wa CCM kutoka wilaya zote za mkoa wa Tanga na wabunge wa mkoa huo katika ukumbi wa CCM jijini Tanga. 
Alisema ndani ya chama cha CCM kuna watu ambao ni watendaji wa serikali ambao hawarekebishiki kwa kuwa wamejificha ndani ya chama ili kuficha mambo yao.
Alisema kuna watu wamo ndani ya CCM wanafanya biashara lakini hawalipi kodi ya mapato serikalini. Samia alikemea tabia hiyo na  kuagiza viongozi wa CCM kuwabana watu hao na kuziba mianya ya kukwepa kodi ili kuongeza mapato ya serikali.
Pia alisema ndani ya chama hicho kuna wanafiki kama mchwa wanafukuta ndani kwa kuharibu chama na kusababisha watu wagombane. Aliwataka watu hao wondoke mapema ndani ya chama ili kuendelee kuwa salama na kuongoza nchi. 
Samia aliwatupia 'dongo' wabunge wa mkoa wa Tanga kuwa ni wavivu na kuwataka wawe wanakwenda kuwatembelea wananchi wao badala ya kukaa tu mijini.
Alisema kuwa hata kama hawana fedha, waende hivyo hivyo kwa kuwa wananchi watawaelewa lakini si kuingia mitini moja kwa moja.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa