Mwandishi wa Habari za Michezo na mdau wa maendeleo ya wilaya ya Handeni, Kambi Mbwana, mwenye fulana ya CCM, akikabidhiwa fomu ya kuwania Ubunge, Jimbo la Handeni Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha Muya, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kulia kwa Mbwana ni Jerome Mhando, mmoja wa wadau waliomsindikiza katika tukio la uchukuaji fomu ya kuwania nafasi ya kuwatumikia wana Handeni. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Kambi Mbwana
ajitosa Ubunge Handeni Vijijini
Na Mwandishi
Wetu, Handeni
MWANDISHI wa
habari za michezo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga,
amejitokeza rasmi katika mbio za kuwania ubunge jimbo la Handeni Vijijini kwa
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Makabidhiano
hayo ya fomu yalifanyika mbele ya Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha
Muya, ikiwa ni siku chache baada ya milango ya uchukuaji fomu za kuwania nafasi
za Ubunge na udiwani kufunguliwa rasmi. Akizungumza
mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mbwana alisema kwamba ameamua kujitokeza
katika mbio hizo za ubunge ili afanyie kwa vitendo yale aliyokuwa anayapenda,
hususan katika suala zima la maendeleo, huku wachache wao wakishindwa kuelewa
faida ya harakati zake, zikiwapo zile za kuitangaza Handeni kwa njia mbalimbali.
Alisema
wilaya yao imekuwa na changamoto kadhaa zinazohitaji nguvu za pamoja katika
suala zima la shida ya kubwa ya maji, migogoro ya ardhi, ukosefu wa huduma bora
za kijamii, hivyo kunahitajika jitihada na mipango ya pamoja kufanikishaji
mambo hayo.
“Nilikuwa
kimya kwa siku kadhaa nikiangalia akina nani wapo katika mchakato wa kuhitaji
nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Handeni Vijijini na kusikitishwa na watu
wasioishi huku na wasiokuwa na uchungu wala dhamira ya kuwakwamua wananchi wakijitokeza
kwa wingi kuwania nafasi ya ubunge, inaonyesha wapo kwa maslahi yao zaidi.
“Hii haiwezi
kukubalika, ukizingatia kwamba wananchi wameendelea kuishi maisha ya mashaka
kwa kukosa maji safi, elimu, afya, michezo, utamaduni na mambo mengine
yanayopaswa kufanyiwa kazi kwa kushirikiana na watu wote, wakiwamo viongozi wa
kisiasa, watendaji wa serikali na Watanzania kwa ujumla,” alisema Mbwana.
Licha ya
kuonekana mpya katika ulingo wa kisiasa hususan kwa nafasi ya ubunge, Mbwana
anakumbukwa na kushukuriwa na wengi kutokana na mradi wake wa Tamasha la
Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka, kuasisi Taasisi ya Handeni
Kwetu Foundation, bila kusahau kuandika kitabu kinachojulikana kama Dira na
Tumaini Jipya Handeni kilichopokewa kwa hisia tofauti, haswa kutokana na
kilichoandikwa kwenye kitabu hicho.
0 comments:
Post a Comment