WANAWAKE wajasiriamali mkoani Tanga wametakiwa kuwekeza kwenye ardhi ili kujikwamua kiuchumi kwani kilimo ni mkombozi katika kuinua uchumi.
Rai hiyo imetolewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku
Gallawa, ambaye amehamishiwa Dodoma, wakati wa ufunguzi semina ya kampeni ya mwanamke na uchumi iliyoandaliwa na kampuni ya Angels Moment kwenye ukumbi wa Naivera.
Gallawa, alisema wanawake wamekuwa wakijishughulisha na shughuli mbalimbali za mikono lakini zimekuwa haziwaletei maendeleo ya haraka.
“Wajasiriamali wa Tanga wanafanya shughuli nyingi za mikono lakini maendeleo hayatokei kwa haraka, hivyo nawaomba nunueni ardhi ambayo ni kitu cha kudumu na kilimo hakimtupi mtu hata siku moja,” alisema Gallawa.
Naye Mkurugenzi wa Kampeni ya wanawake na uchumi, Mahada Erick, alisema wanawake wajariamali wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa mitaji na uwezo mdogo kuzitambua fursa zilizopo katika maeneo yao.
Aidha, alisema kuwa jamii pia imekuwa ikishindwa kuwaunga mkono katika uwekezaji wa rasilimali ardhi, hali ambayo inasababisha kina mama wengi kuogopa kushiriki shughuli za kilimo
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment