Kila hifadhi ya taifa ina upekee wake. Na hicho hukifanya kuwa
kivutio kwa watalii. Hifadhi ya Taifa ya Saadani ina vivutio vya
kihistoria kama vile wanyama, mito na bahari. Nadhani ni hifadhi pekee
inayoweka pamoja vivutio vyote.
Kihistoria Hifadhi ya Saadani inapakana au
kuhifadhi miji ya kihistoria kama Saadani wenywe, Utondwe, Kipumbwi na
Mkwaja, Pangani, Buyuni Ukuu na Buyuni Kitopeni ambayo ingawa sasa
haijulikani tena.
Katika zama zake ilikaribisha wageni wa kimataifa,
au kuwa miji ya kibiashara (ya maliasili na watumwa) na kuwakaribisha
wakoloni na kujenga miji.
Saadani ulikuwa mji mkubwa sana wakati wa ukoloni
wa Wajerumani na pia kaburi la yule mmishenari maarufu aliyekuja kueneza Ukristo, hasa Mombasa, Tanga na Kilindi, Johannes Rebmann liko hapo hadi leo.
wa Wajerumani na pia kaburi la yule mmishenari maarufu aliyekuja kueneza Ukristo, hasa Mombasa, Tanga na Kilindi, Johannes Rebmann liko hapo hadi leo.
Hadi leo Kipumbwi bado ni bandari muhimu ya
majahazi inayounganisha Wazanzibari na Watanganyika kwa kufanya safari
kati ya kijiji hicho cha pwani na bandari kuu ya awali – Mkokotoni.
Safari hizo ziko kila siku.
Miji ya Pangani, Bagamoyo na kijiji kilichopotea
cha Utondwe vina mpatia fursa mtalii kuvifikia wakati anapotembelea
hifadhi hiyo.
Utondwe unaandikwa na Wareno kama mji wa mashamba
ya chumvi na askari wa Kizaramo wapiga mishale wazuri. Ushahidi ni
msikiti wa kale uliopo hadi sasa huko Kitame, ingawa hautumiki.
Saadani ni hifadhi inayopakana na mito mitatu.
Ruvu uko mbali lakini kuna Pangani na Wami. Mito hii mitatu kwa pamoja
hukutana huko baharini na kutengeneza mkondo hatari wa Nungwi unaoleta
vurugu katika majira fulani fulani.
Serikali ya Zanzibar kama ingekuwa na uwezo wa
kifedha ungeweza kutengeneza bomba la kuvuta maji baridi kutoka kwenye
kine kirefu cha Nungwi, yanayotokana na Ruvu, Wami na Pangani, mito
mitatu inayopangana na hifadhi ya Saadani.
Pia, ndani ya mito hiyo unajifunza maisha na uhifadhi unaofanyika wa maisha ya majini na baharini ya wanyama na mimea.
Wakati ukiwa Mto Wami unajifunza maisha ya
baharini na wanyama wake, Mto Pangani una hifadhi kubwa ya mapito ya
kihistoria na biashara- utumwa, katani, mali ya asili, hasa meno ya
tembo na nazi mbichi na mbata.
Ukisafiri katika Mto Pangani hadi huko ndani nchi
kavu unakutana na vituo vya kihistoria ikiwamo mahali Bushiri bin Salim
alipoishi, Matakani na Kijiji cha Bushiri.
- Mwananchi
- Mwananchi
0 comments:
Post a Comment