Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imetakiwa kuvipa kipaumbele vikundi vya ujasiriamali ikiwa na pamoja na kuwapatia elimu ya mafunzo mara kwa mara.
Ushauri huo ulitolewa na Mwalimu wa Vikoba, Rukia Mwinyi wakati wa
mafunzo ya wajasiliamali yaliyofanyika jana jijini Tanga, akisema kuwa
endapo serikali itaweza kutoa elimu hiyo ipasavyo ile sera ya kupambana
na umasikini itafanikiwa.
“Jambo hili likifuatiliwa kwa umakini tutafanikiwa kujikomboa katika
umasikini kwani wajasiriamali waliowengi hasa katika vikundi vyetu
hatuna elimu hii kwa ufasaha ambayo tunaihitaji kwa nguvu zote,”alisema
Rukia.
Aidha, Rukia alisema mafunzo kwa wajasiriamali yamekuwa hayatolewi
mara kwa mara kitendo kinachowafanya kutokuwa na uelewa sahihi juu ya
suala hilo na kushindwa kutimiza malengo waliokusudia.
Awali akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima
Dendego aliwataka kuwa na uchungu na maendeleo ikiwa ni pamoja na
kutangaza fursa za kimaendeleo wanazozifanya ili kufikia lengo la
kuongeza pato la mtu mmoja mmoja.
Dendego alisema mbali na kutangaza bidhaa zao pia wajikite katika
shughuli za kilimo ambazo wataziuza nje ya nchi hususani Kenya ambako
wamekuwa na uhitaji mkubwa wa mazao kama chakula yatayopatikana mkoani
Tanga.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment