Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imesema itawachukulia hatua walimu wote waliojiongezea
madai kwa udanganyifu na kuahidi kuwalipa wale wote wenye madai halali.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa na Waziri wa Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia wakati wa ziara ya kukagua
miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Alisema baadhi ya walimu wamekuwa wakifanya udanganyifu kwa
kujiongezea kiwango cha madai yao kwa serikali, tofauti na madai yao
halali.
Waziri Ghasia alisema tabia hiyo imekuwa ikiikera serikali, kwani
wanachangia kwa kiasi kikubwa kulisababiashia hasara taifa, hali
itakayochangia kurudi nyuma uchumi.
“Walimu tekelezeni wajibu wenu, kwani mpo hapa kwa ajili ya kutoa
huduma bora na stahiki kwa jamii na si kufanya utapeli,” alisema
Ghasia.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Lewis Kalinjuna, alisema wanatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kalinjuna alisema baadhi ya miradi waliyotekeleza ni ujenzi wa
maabara tatu za sayansi katika kila shule ya sekondari pamoja na
kuboresha miundombinu ya maji na afya
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment