Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KATIKA kuelekea kinyang’anyiro cha kumsaka Nice&Lovely Miss
Tanga 2014, washiriki wametakiwa kujiamini na kuongeza juhudi ili
waweze kufanya vizuri katika fainali za shindano hilo kwenye ukumbi wa
Hoteli ya Mkonge, June 21.
Ushauri huo umetolewa na Miss Tanga 2012, Theresia Kimolo, ambaye
alikuwa ni miongoni mwa wapenzi wa tasnia ya urembo mkoani Tanga
waliojitokeza kushuhudia mazoezi ya warembo wanaowania taji hilo
yanayofanyika kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort, chini ya Mwalimu wao
Mariam Bandawe.
Alisema, washiriki hao hawana budi kuzidisha uelewa kwenye maeneo
mbalimbali, ikiwemo kujieleza, kutabasamu na kutembea mbele za watu,
lengo likiwa kuleta ushindani wakati wa maandalizi yao na hata hatua ya
kumsaka bingwa wa kinyang’anyiro hicho.Awali, akizungumza mara baada
kumalizika mazoezi hayo, Mratibu wa shindano hilo, Benson Jackson
alisema, maandalizi ya kuelekea shindano hilo yamekamilika kwa asilimia
kubwa. kwa warembo hao kufanya maandalizi kila siku.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment