Home » » BABU AMBAKA MJUKUU WAKE

BABU AMBAKA MJUKUU WAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MTOTO wa miaka saba wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mkata wilayani Handeni, Tanga amebakwa na babu yake na kumsababishia maumivu makali na kumwagika damu nyingi.
Tukio hilo lilibainika wakati mtoto huyo akiwa darasani na wenzake ambapo alianza kuvuja damu nyingi hali iliyowafanya wanafunzi wenzake kutoa taarifa kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Moses Kimlayi, aliyefika kushuhudia tukio hilo.
Baada ya kupewa taarifa hiyo Mwalimu Kimlay alimkabidhi mwanafunzi huyo kwa walimu wa kike kwa lengo la kumchunguza kama kweli kuna unyama aliofanyiwa. Baada ya kumhoji mwanafunzi huyo alisema babu yake alimbaka na kumtishia asimueleze mtu yeyote.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa