Home » » WAJASIRIAMALI MKATA WAPATIWA ELIMU

WAJASIRIAMALI MKATA WAPATIWA ELIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
AtomtekSHIRIKA la Atomtek Nuclear Energy limetoa msaada wa kielimu kwa kikundi cha kinamama wajasiriamali kilichopo Kata ya Mkata, Mkoa wa Tanga kwa lengo la kuwainua kiuchumi na kuondokana na umasikini.
Hayo yalibainishwa na Ofisa Habari wa shirika hilo lenye makao yake Makuu Makuu nchini Uturuki, Yusuph Mjema alipofanya ziara yake ya siku moja ya kukitembelea kikundi hicho, ili kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao ujasiliamali.
Katika hafla hiyo, Mjema alisema shirika lao limeamua kuwatembelea kinamama hao baada ya kufanya uchunguzi na kubaini wanakabiliwa na changmoto nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu ya biashara ndogondogo, hali inayocahngia biashara zao kukwama.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa