Home » » Wanafunzi wavamia hospitali

Wanafunzi wavamia hospitali

Askofu wa Kanisa la Aglikana Jimbo la Tanga, Mahimbo Mndolwa
 
Wanafunzi wanaosoma kozi ya mwaka mmoja ya Medical Attendant katika chuo cha St. Augustine Muheza, juzi walivamia ofisi za uongozi wa hospitali Teule Muheza wakidai kurudishwa fedha zao za ada wakidai kozi hiyo ya mwaka mmoja haijasajiliwa na wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii haitambuliki.
Zaidi ya wanafunzi 460 walivamia na kutaka kuchoma hospitali hiyo.
Wanafunzi hao walikuwa wakisema kuwa wamepata taarifa kwamba kozi hiyo haijasajiliwa wizarani na wala haifahamiki na kwamba fedha zao za ada zimekwenda bure.

Mmoja wa wanafunzi hao ambaye aliomba jina lake listanjwe aliwaambia waandishi wa habari kwamba hapo mwanzo walikuwa wanavaa sare za chuo, lakini cha kushangaza hivi karibuni wamezuiwa wasivae wakidai kuna wakaguzi walifika wakauliza waliyovaa sare zile ni kina nani.

Alisema pia waliambiwa kuwa kozi hiyo itamalizika Aprili mwaka huu, lakini baadaye wakaambiwa kuwa itamalizika Machi, kitu ambacho wanashindwa kuelewa.

Wanafunzi hao walisikika wakisema wanamtaka Askofu wa Kanisa la Aglikana Jimbo la Tanga, Mahimbo Mndolwa, ambaye kanisa lake ndilo linalomiliki chuo hicho kueleza ukweli kuhusu kozi hiyo kama mmoja anaitambua ama la.

Walisema kuwa kama hawataelezwa ukweli, wataandamana hadi kwa mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na kwa Rais Jakaya Kiwete. Mganga Mfawidhi wa
Hospitali Teule wilayani Muheza, Dk. Rajabu Mlahiyo, hakupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa safarini kikazi.

Wanafunzi hao wanalipa kozi ya mwaka mmoja Sh. 600,000 na sare wanashona wenyewe.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa