TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Tanga,
wametakiwa kuchunguza ufisadi unaofanyika kwenye halmashauri zote za
mkoa huo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watakaobainika.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, wakati
wa sherehe za kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014
zilizoandaliwa na taasisi hiyo mwishoni mwa wiki na kueleza kuwa kuna
ufisadi unaotendeka kwenye halmashauri hali inayosababisha kudumaza
juhudi za maendeleo zinazofanywa na serikali kuu.
Aliitaka TAKUKURU kufanya kazi yake kwa uadilifu ili kuwabaini mchwa
wote, hasa watendaji wenye mamlaka waliopo kwa ajili ya kuchota fedha
za wananchi kwa manufaa yao.
“Hatuwezi fika tunakokutaka iwapo kuna wachache wetu wanakwamisha
jitihada za kujiletea maendeleo kwa ubinafsi na kupenda kujilimbikizia
mali kwa njia isiyo halali ikiwemo rushwa za miradi ya maendeleo,”
alisema Gallawa.
Hata hivyo, Kamanda wa TAKUKURU mkoani hapa, Edson Makallo, alisema:
“Serikali peke yake haiwezi kumaliza rushwa katika nchi hii bila
kushirikisha wadau kama mahakama, polisi na wanasheria. Lazima tuongee
lugha moja ya kuhakikisha tunapigania jambo hili kwa uadilifu.”
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment