Mkuu wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Hafsa Mtasiwa
Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Hafsa Mtasiwa wakati akifunga mafunzo ya 15 ya mgambo yaliyofanyika katika kijiji cha Slabu Azimio kilichopo Kata ya Mikinguni Tarafa ya Mwera Wilayani Pangani.
Mtasiwa alisema mafunzo ya mgambo ni muhimu kwa wananchi na kuyafananisha na ajira binafsi na kuelezea athari kubwa zinazoweza kupatikana endapo mbinu za kivita wanazozipata watazitumia kwa uharifu.
“Vijana msikubali kutumika vibaya kisiasa ama katika makundi ya uharifu kwani nyinyi ni tegemeo kubwa la taifa hili.. msijihusishe na matendo ya uovu kama vile ujambazi na ugaidi, ” alisema Mtasiwa.
Aliwataka wahitimu hao kuzitumia vema fursa za ajira katika majeshi kwa kujitokeza kuomba pamoja na kujiendeleza kielimu ili waweze kufaidika na ushindani wa soko la ajira badala ya kulalamikia serikali.
Awali wakisoma risala kwa Mkuu huyo wa Wilaya, wahitimu hao, walieleza changamoto mbalimbali ikiwamo ugumu wa kupata ajira katika majeshi na ukata wa fedha za kuendeshea mafunzo hayo.
Katika risala hiyo iliyosomwa na mhitimu, Asia Daffa, waliiomba halmashauri ya wilaya hiyo kutenga fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kugharamia mafunzo hayo na serikali kutoa kipaumbele cha ajira katika majeshi kwa vijana waliyopitia jeshi la mgambo au Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya Pangani, SGT Mwinjuma Chakaya alieleza kuwa mafunzo hayo ya 15 kwa mwaka 2013/2014 yalianza na vijana 55, kati ya hao, waliohitimu ni 51 .
Alisema vijana hao kwa kipindi chote walijifunza masomo mbalimbali ikiwamo kupiga kwata, mbinu za kivita, usomaji ramani, uokoaji, nidhamu, uadilifu na jinsi ya kujitegemea kabla ya kupata ajira mahali popote.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment