Home » » CCM TANGA YAWAKEMEA VIONGOZI MIUNGU WATU

CCM TANGA YAWAKEMEA VIONGOZI MIUNGU WATU

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) Mkoa wa Tanga imekemea tabia ya watendaji wa serikali wanaojifanya miungu watu na kuzitaka mamlaka husika kuhakikisha wanawachukulia hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Uamuzi huo ulifikiwa juzi wakati wa kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe kutoka wilaya zote za mkoa huu, ambapo mambo mawili yaliyotawala ni migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na mgogoro kati ya wakulima wa chai, chama cha wakulima wa chai (Utega) na mwekezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa CCM Tanga, Gustav Mubba, alisema viongozi wa serikali wanaopewa mamlaka ya kuwaongoza wananchi wanashindwa kufanya kazi zao ipasavyo na kuendekeza tabia ya kuwanyanyasa badala ya kuwaondolea kero zao.
Mubba alisema viongozi wa ngazi za chini wameshindwa kuwajibika kwa kuwa mstari wa mbele kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wananchi bali wanachangia kuwepo kwa migogoro kwenye maeneo yao kwa kutokuzingatia namna ya utoaji wa ardhi kisheria na kuwafanya wananchi kuwatupia lawama viongozi wao.
Alisema kitendo hicho kimeleta manung’uniko kwa wananchi wa wilaya za Kilindi na Handeni, hali iliyowafanya kuichukia serikali yao.
Aidha, katibu huyo alisema kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2014/2015 viongozi wa vijiji, madiwani na wabunge watapimwa kwa kazi walizofanya.
Akizungumzia suala la mgogoro wa wakulima wa chai, chama cha wakulima na mwekezaji, Mubba alisema halmashauri hiyo imeunda kamati ya watu saba kuonana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kuangalia namna sahihi ya kumaliza mgogoro huo.

CCM Tanga yawakemea viongozi miungu watu

Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa