WATU wawili wamefariki dunia hapo hapo na wengine wanane kujeruhiwa vibaya, baada ya gari aina ya Noah walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori aina ya Volvo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, athibitisha kutokea tukio hilo jana na kueleza tukio hilo lilitokea saa 5 asubuhi, wakati Noah yenye namba za usajili T266 AXZ lililokuwa likitokea Kabuku kwenda Mkata, lilipokuwa likijaribu kulipita lori hilo kwa mwendo kasi.
Kamanda Massawe, alimtaja dereva wa Noah kuwa ni Abdallah Selehe (60), mkazi wa Hale, wilayani Korogwe.
Alisema dereva huyo, amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga na mpaka jana jioni alikuwa hajitambui kutokana na kupoteza fahamu.
Aliwataja watu waliofariki dunia, kuwa ni wanawake wawili, lakini majina yao yalikuwa hayajatambuliwa.
Alisema chanzo cha ajili hiyo, ni dereva wa Noah kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake kwenye kona.
“Ajali nyingi zinatokea kutokana na madereva kutokuwa makini, kwani wengi wao wanasababisha ajali hizo kwa kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yao bila kufikiria kufanya hivyo ni kukiuka sheria za usalama barabarani,” alisema Kamanda Massawe.
Chanzo:Mtanzania

0 comments:
Post a Comment