Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MRATIBU
wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana,
amesema kwamba tamasha lao haliwahusu watu wa Handeni tu, badala yake
juhudi zinafanyika kupata watu mbalimbali, wakiwamo kutoka wilaya za
Korogwe ili kuleta picha ya kimkoa.
Tamasha hilo lililoanza kugusa hisia za wengi limepangwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu huku likiwa na lengo la kutangaza utamaduni wilayani humo na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Mbwana, alisema mbali na vikundi vya Handeni, pia itakuwa jambo la busara kama watapata washiriki wengine nje ya wilaya hiyo kwa ajili ya kuleta mvuto zaidi.
Alisema wasanii waliokuwa katika wilaya Korogwe, Kilindi na kwingineko katika mkoa huo wa Tanga, ni jambo la muhimu kuwakusanya pamoja kwa ajili ya tukio hilo.
“Itakuwa ajabu kama tunapozungumzia utamaduni wa Handeni, tutawaacha nyuma wenzetu wa Kilindi ukizingatia kuwa awali walikuwapo wilaya moja, hivyo kuna umuhimu kushirikiana nao.

“Kuna
vikundi vizuri ambavyo tunatarajia tutakuwa navyo kutoka katika wilaya
hizo, ukizingatia kuwa lengo letu ni zuri na hakuna sababu ya kujitenga
katika mambo haya ya kimaendeleo,” alisema.
Wadhamini
waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Phed Trans
inayomilikiwa na Yusuphed Mhandeni, Grace Products, Screen Masters,
Dullah Tiles $ Construction Ltd, Katomu Solar Specialist na Country
Business Directory (CBD).
Wengine
ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, SmartMind & Partners chini
ya ANESA COMPANY LIMITED, ikidhamini kwa kupitia kitabu cha ‘NI WAKATI
WAKO WA KUNG'AA, Screen Masters, Saluti5.com, Lukaza Blog, Kajunason
Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu Blog.
0 comments:
Post a Comment