WAZAZI na walezi ni chanzo kikuu cha ongezeko la
watoto waishio katika mazingira magumu hapa nchini.
Hayo yalisema jana na katibu wa kikundi cha Mtandao
wa Marafiki wa Elimu Mwangaza, Ayub Bwanamad, alipozungumza na mwandishi wa
habari hizi mjini Pangani jana.
Alisema ugumu wa maisha kwenye baadhi ya familia
unageuzwa sababu ya ongezeko la watoto hao huku akizitaka ofisi za kata kuweka
utaratibu maalumu wa kuwasaidia.
Alishauri ofisi za wakuu wa Idara ya Maendeleo ya
Jamii kutenga bajeti ya kuwasomesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu
ili kupunguza changamoto huku akibainisha kwamba yapo maeneo mengine hayafikiwi.
Hata hivyo, Bwanamad ameitaka jamii kuacha kuwapa
kazi ngumu na zenye kudhalilisha watoto kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwanyima
haki zao za msingi na kukiuka sheria.
Kwa mujibu wa katibu huyo kumjenga mtoto kwenye
mazingira bora na kuwa karibu naye itapunguza wimbi hilo la watoto wanaoishi
katika mazingira magumu huku akitoa wito kwa walezi na wazazi kuwapenda na
kuwafundisha maadili mema watoto wao.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment