KONGOZI wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe, amesema
anaisikitikia serikali kwa kutumia fedha nyingi kuliendesha Shirika la
Umeme nchini, TANESCO. Kauli hiyo aliitoa katika kampeni za uchaguzi wa
udiwani katika Kata ya Genge, wilayani Mheza.
Mbowe alisema serikali hutumia jumla ya Sh trilioni 2.8, fedha zinazotokana na makusanyo ya kodi za wananchi kwa ajili ya kuendesha Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO kwa mwaka.
Alisema fedha hizo zinatumika katika kuendeshea mitambo ya shirika hilo kwa kuyalipa makampuni yanayozalisha umeme pamoja na kununua mafuta mazito kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kuzalishia nishati ya umeme nchini.
Mbowe alisema kwa siku moja pekee shirika hilo hutumia jumla ya Sh bilioni 5.4 kwa ajili ya kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme.
“Nashangazwa na serikali hii isiyosikivu, inatumia kodi za wananchi katika kulipa makampuni yatuzalishie umeme wakati vipo vyanzo vya uhakika vya maji ambavyo vina gharama nafuu.
“Umeme umekuwa ukitumiwa na viongozi wakubwa nchini kama biashara, kwani kunatumika pesa nyingi kuzilipa kampuni zao ambazo wanasema ni kampuni za kigeni zimekuja kuwekeza kwenye nishati hiyo hapa nchini,” alisema Mbowe.
Alisema inauma kwa kuona robo ya makusanyo ya mapato ya ndani inakwenda kwenye umeme badala ya fedha hizo kutumika kuwekeza kwenye elimu, afya na muindombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali nchini.
Akiongelea uhaba wa maji wilayani humo, alisema udhaifu wa viongozi wa ngazi ya wilaya ndio umesababisha kero hiyo kuwa sugu.
“Wananchi wa Muheza mna kazi moja tu ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani ili muweze kuunganisha nguvu za maendeleo zinazofanywa na CHADEMA katika mikoa mingine nchini kwa sasa,” alisema Mbowe.
Hata hivyo mgombea wa udiwani wa Kata ya Genge, Josepha Komba (CHADEMA), alisema iwapo watakubali mabadiliko ya uongozi katika kata hiyo, basi kuna uwezekano mkubwa wa kata hiyo kuwa na maendeleo makubwa katika kipindi kifupi kijacho.
“Ndugu zangu tukubali kubadilika, kwani inawezekana Kata ya Genge kuwa na shule yake, zahanati yake pamoja na huduma ya uhakikia ya maji iwapo tutakubali mageuzi na kuondokana na fikra hasi dhidi ya upinzani.

0 comments:
Post a Comment