Home » » Maelfu ya Watanzania wamzika Marehemu Sharo Milionea jijini Tanga jana.. Tazama hapa

Maelfu ya Watanzania wamzika Marehemu Sharo Milionea jijini Tanga jana.. Tazama hapa

Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea enzi za uhai wake.
Waumini wa Kiislam wakiwa katika Ibada ya Kuuswalia Mwili wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea aliefariki kwa ajali ya Gari hivi karibuni huko Muheza,Mkoani Tanga.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea likiwasili Nyumbani tayari kwa Taratibu za Mazishi yaliyofanyika leo kwenye Kijiji cha Lusanga,Wilayani Muheza,Mkoani Tanga.
udogo ukitupiwa kaburini wakati wa mazishi ya Msanii wa Muziki na Filamu hapa nchini,Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea,ambayo yalihudhuliwa na Watu mbali mbali hapa nchini,wakiwemo viongozi katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Muigizaji Maarufu hapa nchini,Mzee Athuman Amri a.k.a King Majuto ambaye ni Baba Mdogo wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea akitupa mchanga kaburini wakati wa Mazishi ya Sharo yaliyofanyika leo katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Vijana wakiwa wamepanda mnazi kuona mazishi ya Msanii wa Muziki hapa nchini,Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Waombolezaji wakimsaidia mwenzao aliyepoteza fahamu msibani.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akitoa pole za Chama mara baada ya kumalizika kwa mazishi ya Msanii wa Muziki na Filamu,Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Kiongozi wa Tanzania Fleva Unit,Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za EOTF.
Baadhi ya wasanii msibani, Lusanga.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mbando (katikati) akiwa pamoaja na baadhi ya wasanii wa Muziki wa BongoFleva wakati wa Mazishi ya Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.Picha na Bashir Nkoromo.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa