Home » » WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA


Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Ukanda wa Uwekezaji wa Kiuchumi wa Mkoa wa Tanga Bw Chris Chae. Uwekezaji mkubwa unatarajiwa kuanza katika eneo hilo hivi karibuni.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akionesha kukubaliana na Maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha kuzalisha mifuko na maturubai cha Pee Pee kilichopo Mkoani Tanga.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda( Katikati), Mkuu wa Wilaya ya Tanga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Bi Halima Dendegu na watendaji wengine wa Mkoa Tanga wakipokea taarifa ya hali ya mgodi wa malighafi za kuzalisha saruji ya Lime stone unaomilikiwa na kiwanda cha Saruji Tanga.
Mashine za kisasa za kusaga na kupanga unga katika Viwango mbali mbali zilizopo katika Kiwanda cha Unga cha Pembe kilichopo Mkoani Tanga.
Mgodi wa malighafi za kuzalisha saruji( limestone) ambao umekuwa ukitoa malighafi hizo tangu kuanzishwa kwa Kiwanda hicho miaka zaidi ya 30 iliyopita. Tafiti zinaonesha kuwa, malighafi hiyo itaendelea kupatikana kwa zaidi ya miaka 130 ijayo.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa