Na Amina Omari, Tanga
HALMASHAURI zimetakiwa kutenga fedha kwa ajili ya kusimamia mpango wa utekelezaji wa maduka ya dawa muhimu, kwa lengo la kuhakikisha huduma ya dawa inapatikana kwa wakati hasa maeneo ya vijijini.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli, wakati akifungua mkutano wa wadau wa mpango wa maduka ya dawa muhimu.
Alisema ipo haja ya halmashauri kujiwekea utaratibu na sheria za ukusanyaji fedha kwa ajili ya mpango huo badala ya kutegemea wahisani ambapo wakati mwingine fedha zinachelewa huku huduma zikikosekana.
Alisema lengo la Serikali ni kuboresha huduma ya upatikanaji wa dawa iwe karibu na wanachi kwa kupitia maduka ya dawa muhimu, pamoja na vituo vya afya na hospitali zote nchini.
Alisema licha ya juhudi nyingi zinazochukuliwa kwa kuanzisha mifuko ya uchangiaji kwa jamii, lakini bado dawa hazipatikani kwa wakati hususani maeneo ya vijijini hali inayowafanya wananchi kununua kwa watu binafsi.
Alisema ipo haja ya Baraza la Famasia kufanya tathimini ya changamoto zinazoikabili sekta ya afya kwa ajili ya kubaini kasoro zilizopo na kuzifanyia kazi ipasavyo.
“Naagiza Baraza kufanya tathimini na ufuatiliaji wa mpango wa maduka ya dawa muhimu, kwa ajili ya kubaini changamoto zake na kuzitatua kwa lengo la kuleta tija ya mpango huo kwa wananchi,” alisema Kikuli.
Awali, Msajili wa Baraza la Famasia Tanzania, Mildred Kinyawa, alisema mpango huo unalenga kuboresha huduma za utoaji sahihi wa dawa kupitia sekta binafsi katika maeneo ya vijijini na miji midogo.
Alisema mpango huo unalenga kuondoa matatizo yaliyokuwa yakifanywa na watoa dawa katika maduka ya dawa kwa kuwa na wauzaji wasio rasmi wala ujuzi na utaalamu huo kwa kuuza dawa zilizosajiliwa na zisizosajiliwa.
Naye, Mkurungezi wa Huduma na Uendeshaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Sikubwabo Ndendabanka, alisema mpango huo utasaidia kupunguza maduka ya dawa yanayoendeshwa bila vibali, uuzwaji wa dawa za wizi na bandia na kugeuzwa kuwa vituo vya kutolea tiba.
Alisema kabla ya mpango huo, maduka hayo yalichangia kuhatarisha maisha ya Watanzania kwa uuzwaji wa dawa holela na hata yale yaliyopigwa marufuku.
“Hadi sasa chini ya mpango huo tumeweza kutoa mafunzo kwa wamiliki wa maduka ya dawa muhimu 13,023 watoa dawa 11,872 na maduka 4,395 yamefunguliwa katika mikoa 21 ya Tanzania,” Alisema Ndendabanka.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment