Taarifa zilizo na mahusiano na picha hapo juu zilizokutwa maeneo ya kata ya Msambweni mjini Tanga. Wanachama wa CUF waliamua kutumia jeneza bandia na kinyago cha maiti kuonyesha hisia zao za kufurahia ushindi wa kata hiyo walio upata kwenye uchaguzi uliofanyika huko. sidhani kama ni vizuri tukifikia huku! Ushabiki wa namna hii unaweza kuleta chuki na madhara, ni haki yao CUF kuonyesha furaha yao ila kwa jinsi hii haipendezi! kuweka picha ya mgombea wa CCM aliyeshindwa kwenye uchaguzi kwenye mfano wa jeneza bandia tena huku wakiweka sania ambalo kila anae pita njia anatupia pesa kama rambirambi haipendezi na sidhani kama ushabiki huu unafundisha kitu.
Kwa Tukio zaidi ingia hapa: CHINGA ONE BLOG
0 comments:
Post a Comment