Home » » Makusanyo ya mapato yapanda Lushoto

Makusanyo ya mapato yapanda Lushoto

HALMASHAURI ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, imefanikiwa kuongeza kipato chake cha mapato ya ndani kwa zaidi ya Sh milioni 800 katika mwaka wa fedha 2012/13. Ongezeko hilo, limetoka Sh milioni 500 zilizokusanywa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/2012.

Hayo yameelezwa na Mweka Hazina wa Wilaya hiyo, Hafidhi Mohamed, wakati akiwasilisha taarifa ya hesabu za Halimashauri kwa mwaka wa fedha 2012/ ulioishia Juni 2013 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani jana.

Alisema kiwango hicho cha mapato kimeongezeka kutokana na kuongeza ushuru wa kodi za viwanja, vibanda vya biashara pamoja na kodi za mazao wanayouza nje ya wilaya hiyo kwa wingi.

Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo hilo, Henry Shekifu, aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha wanaendelea kusimamia kwa ukaribu vyanzo vya mapato ya ndani pamoja na kuongeza vyingine ili Wilaya hiyo iweze kujiletea maendeleo kutokana na makusanyo hayo.

Naye Mkurungezi Mtendaji, Jumanne Shauri alisema tayari wametenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kitega uchumi cha biashara ambapo iwapo watapata mwekezaji wa kujenga au kuingia naye ubia, kiwango cha mapato kitaweza kuongezeka hadi kufikia zaidi ya asilimia 100 pamoja na kuboresha maeneo ya masoko ya mazao.
Chanzo: Rai

1 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa