Home » » Shehena ya Bidhaa yakamatwa Bandari Bubu Tanga

Shehena ya Bidhaa yakamatwa Bandari Bubu Tanga

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Shehena ya bidhaa mbalimbali yenye thamani ya mamilioni ya Shilingi ikiwemo vipuri vya magari kutoka nchini tofauti zimekamatwa katika bandari bubu ya Kigombe iliypo wilayani Muheza Mkoani Tanga wakati ikiingizwa nchini Kinyume cha Sheria.
Kaimu Kamanda mkoa wa Tanga mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mayala Towo
Akizungumza katika eneo la tukio Kaimu Kamanda mkoa wa Tanga mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mayala Towo amesema shehena hiyo ilikua pia na mafuta ya kupikia kutoka ubelgiji,Sukari kutoka India na vipuri kutoka nchi tofauti za Ulaya.
Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) tawi la Tanga Bwana Samir Buelgaaba amekiri kuwa hali ya ukwepaji wa kodi katika bandari bubu ya Kigombe ni ya kutisha kwa sababu sehemu kubwa ya bidhaa zinazouzwa katika maduka mbalimbali katika baadhi ya maduka yaliyopo katika jiji la Tanga, Muheza na Mkinga zinatoka nje ambazo inadaiwa kuwa zimeingizwa nchini kinyume cha sheria.
Kufuatia hatua hiyo kaimu meneja wa forodha mkoa wa Tanga Bwana Jumbe Magoti amesema wazingatia sheria zilizowekwa katika zoezi la tozo za faini kisha watataifisha vyombo vilivyotumika katika usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka kisiwani Zanzibar kuingizwa bara bila kulipiwa ushuru.

Chanzo: East Africa Tv

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa