Home » » WATAALAM WAJADILI KUKABILIANA NA INZI MUHARIBIFU

WATAALAM WAJADILI KUKABILIANA NA INZI MUHARIBIFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Akielezea hali ya uharibifu unaofanywa na inzi huyo, Ofisa Mradi wa Muungano waWajasiliamali Vijijini (MUVI), Edwin Shoo alisema, wakulima wa machungwa wa wilaya za Muheza, Handeni na Korogwe uzalishaji wao umeshuka kwa asilimia 50 baada ya kuharibiwa na mdudu huyo.
Alisema kuwa mdudu huyo amekuwa akiharibu matunda hayo hatua ambayo imechangia wakulima wengi kukata tamaa katika kulima mazao hayo.
Naye kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Handeni, Ezekieli Munike, alisema ujio wa mdudu huyo ni tishio kwa wakulima huku dawa zikiuzwa kwa bei ya juu.
Alisema kuwa kutokana na tafiti zilizofanywa ilibainika kuwa inzi hao wametokea nchi jirani ya Kenya ambao hutaga mayai yao ndani ya tunda na kuliangusha tunda hilo.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa