Home » » SWALA YAKAMILISHA UTAFITI PANGANI

SWALA YAKAMILISHA UTAFITI PANGANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi Mtendaji wa Swala, Dk. David Ridge
KAMPUNI ya mafuta na gesi ya Swala hapa nchini  imetangaza kukamilika utafiti wa kupata nishati hiyo uliyoanza Agosti 24 mwaka huu bonde la mto Pangani Tanzania uliohusisha kilomita 200 .
Akizungumzia juu ya kukamilika kwa utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Swala, Dk. David Ridge,   alisema utafiti wa bonde la Pangani umefanyika kwa haraka na ndani ya bajeti iliyopangwa.
Mkurugenzi huyo, alieleza kitakachofuata ni kutambua maeneo yenye uwezo kuchimbwa visima kwa ajili kukamilisha zoezi la awamu ya pili ya shughuli hiyo.
“Kutokana na utafiti huo kukamilika, kampuni hiyo imebainisha kuwa idadi na uwezo wa mifumo iliyotumika pembezoni mwa bonde hilo, inatarajiwa  kutoa malengo ya mpango wa uchimbwaji visima  2015,” alisisitiza Dk. Ridge.
Aidha, Dk. Ridge, alibainisha kuwa baada ya kukamilika kwa shughuli za bonde la Pangani,  mkandarasi atahamia mto Kilombero, Kilosa mkoani Morogoro ambako watafanya utafiti mwingine utakaohusisha kilometa 430.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa