Home » » Wajawazito acheni dawa za kienyeji’

Wajawazito acheni dawa za kienyeji’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
KINA mama wilayani hapa wametakiwa kuacha kutumia dawa za kienyeji ili kuendeleza uchungu wa kujifungua pindi wanapokuwa wajawazito.
Wito huo ulitolewa mjini hapa jana na Mratibu wa Afya ya Uzazi Wilaya ya Muheza, Agness Mbwana, kwenye sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe kwa Uzazi Salama.
Alisema uchungu wa dawa za kienyeji unakuja kwa kasi, hivyo husababisha upasuko wa njia ya kutoka mtoto na hata nyumba ya uzazi na mtoto kufa.
Mbwana alisema athari nyingine ni mama kutokwa na damu nyingi, kitu ambacho kinaweza kusababisha kupoteza maisha.
Alisema kuwa tatizo jingine kina mama wana tabia ya kujiamini.
Hata hivyo, Mbwana alisema kwa sasa kuna mafanikio makubwa, kwani kina mama wana uelewa wa kujifungulia katika vituo vya afya.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ambae aliwakilishwa na Katibu Tawala Wilaya, Paul Moshi, alisema serikali inaahidi kutoa ushirikiano katika kutoa vifaa tiba na kinga, ili kusaidia kutoa huduma bora kwa wateja.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa