Home » » Mombo wamuomba JK atekeleze ahadi zake

Mombo wamuomba JK atekeleze ahadi zake

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Rais Jakaya Kikwete
 
Wakazi wa mji mdogo wa Mombo Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, wamemtaka Rais Jakaya Kikwete, atoe tamko kuhusiana na ahadi alizotoa wakati wa kampeni mwaka 2010 kuhusu kero mbalimbali za mji huo zitatekelezwa lini.
Rais Kikwete alitoa ahadi hizo wakati wa mikutano ya hadhara ya kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Pamoja na mambo mengine, Rais aliwaahidi wananchi hao kuwa atahakikisha kwamba Mombo inakuwa halmashuri kamili ya mji, kilimo cha umwagiliaji katika mto Mkomazi na maji ya uhakika kwa wakazi wa maeneo hayo.

Wananchi hao walitaka kujua sababu za kutotekelezwa kwa ahadi hizo na lini zitatekelezwa  kwa kuwa ni ahadi aliyoitoa mwenyewe wakati akiomba kura kwenye mikutano ya kampeni.

Akijibu hoja hizo, Rais Kikwete aliwaeleza wananchi hao kuwa kama alivyowaahidi atahakikisha halmashauri ya mji wa Mombo inapanda hadhi na kuwa halmashauri kamili.

Kuhusu kero ya maji alisema tayari serikali imeshajiandaa katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo zaidi ya Sh. milioni 600 zimetengwa kwa ajili hiyo.
Juu ya umwagiliaji mto Mkomazi, Rais Kikwete aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuanza kazi ikiwa ni pamoja na kuwalipa fidia watu ambao maeneo yao yatachukuliwa kwa ajili ya kutekeleza mpango huo.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa