Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza na wajumbe wa kamati
ya utekelezaji ya umoja huo wilaya ya Lushoto(UVCCM)wakati wa ziara yake ya
kwanza ya kukagua na kuangalia uhai wa umoja huo pamoja na kufanya mikutano ya
hadhara inayofanyika mkoa mzima wa Tanga.
Makange alisema katika dhama hizi za utandawazi vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kubuni miradi mbalimbali ikiwemo kufanya biashara na kufungua makampuni ambayo yataweza kutimiza ndoto zao katika maisha.
Aidha aliwaataka vijana kuangalia changamoto waliokuwa nazo
ili kuweza kukabiliana nazo na kuzipatia ufumbuzi lengo likiwa kuhakikisha
umoja huo unaimarika na kuwataka vijana walipo vyuoni kujitahidi kuingiza
wanachama wapya katika maeneo yao.
Mwenyekiti huyo aliwataka vijana hao kuwa mstari wa mbele
kukitetea chama hicho na kujenga mshikamano na kuachana na makundi yasiyokuwa
na tija lengo likiwa ni kuimarisha umoja huo mkoani hapa.
Na Oscar Assenga, Lushoto.
Chanzo;tanga raha blog
0 comments:
Post a Comment