Home » » Mchezo wa bao marufuku muda wa kazi Handeni – Gondwe

Mchezo wa bao marufuku muda wa kazi Handeni – Gondwe


Na Godfriend Mbuya
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amepiga marufuku wananchi wa wilaya yake kucheza mchezo wa bao na ‘pool table’ wakati wa mchana ambapo ni muda wa kufanya kazi na kutekeleza falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya ‘Hapa Kazi Tu’

Gondwe ameyasema hayo alipofanya mazungumzo maalumu na kipindi cha SUPAMIX kinachorushwa na kituo cha East Africa Radio ambapo amesema baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli na kuanza kazi kuwa Mkuuu wa Wilaya hiyo alikuta muamkoa wa vijana katika kufanya kazi ni mdogo huku wengi wakishinda vijiweni kwa kucheza pool table na bao jambo ambalo amepiga marufuku wakati wa kazi.

“Nimekataza vijana kucheza michezo hiyo wakati wa kazi na nimewahamasisha kushiriki shughuli za ufugaji na  kilimo ambapo wilaya ya Handeni inakubali sana  kilimo cha matunda, alizeti, ufuta na ufugaji wa mbuzi na kuku ambapo kwa kushirikiana na idara ya ardhi tumekubaliana kutenga maeneo ya uwekezaji kwa vijana ambapo serikali itawawezesha kuweza kuyafanyia kazi za kilimo’’ Amesema Gondwe.

Aidha Mkuu huyio wa Wilaya amewataka vijana kujiunga katika makundi ili waweze kupata fedha ambazo kila halmashauri imetakiwa kutenga asilimia 5% ya mapato yake kwa ajili ya vijana na 5% kwa ajili ya wanawake ili waweze kutumia mikopo watakayopata kujikwamua kimaisha kwa kufanya shughuli mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa