Home » » Waandishi wa habari kutoka taasisi ya Malaria no More wawasili Tanga

Waandishi wa habari kutoka taasisi ya Malaria no More wawasili Tanga

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

be1 
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
be2 
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
be3Mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Lyndsey Wajert akiwa tayari kufanyiwa vipimo vya malaria na Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha wakati wa ziara ya waandishi wa Habari hao ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
be4 
Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi anayefanya kazi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Katy Migiro wa Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara mkoani Arusha kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
be5 
Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari uwanja wa ndege wa Arusha kwa safari ya kuelekea mkoani Tanga.
be6 
Eneo la ukingo wa Bahari ya Hindi mkoani Tanga ambapo karibu na eneo walipofikia waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara yao mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Tanga)

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa