Home » » WALIMU WANAOBEZA ELIMU BURE KUKIONA.

WALIMU WANAOBEZA ELIMU BURE KUKIONA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza. 

Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza ametangaza ‘vita’ dhidi ya walimu watakaobainika kutofundisha kwa wakati darasani kwa kisingizio cha mpango wa Serikali wa elimu bure.

Mahiza alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao alichoitisha kwa ajili ya kuweka mikakati ya kikazi na wakuu wa shule, wakurugenzi wa halmashauri na maofisa elimu wa sekondari mkoani Tanga.

Alisema baadhi ya walimu katika shule za msingi na sekondari wamekuwa wakitegea kufundisha na wanapofuatwa na wanafunzi huwajibu hiyo ndiyo elimu bure. “Wanawaambia wanafunzi subirini tu mtaisoma namba mwaka huu,” alisema Mahiza.

Alisema lugha hizo za kuwasimanga wanafunzi ni sawa na kuidhalilisha Serikali jambo alieleza kuwa hatakubali litokee tena.
“Nitawaweka kizuizini walimu watakaotegea au kubainika kutoa lugha za kuitusi Serikali kuhusu mpango wa elimu bure, nitatumia Sheria Namba 8 ya Usalama ya Mwaka 2010 kwani huko ni kuhujumu elimu,” alisema Mahiza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene alisema Serikali imetenga Sh131.4 bilioni ikiwa ni fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule, chakula, mitihani na fidia ya ada.

Alisema Serikali imejipanga kugharamia uendeshaji wa shule ili kuziba pengo la ada na michango mbalimbali iliyokuwa inatolewa na wazazi na walezi.
CHANZO: GAZETI LA MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa