Home » » HANDENI MJINI KURUDIA KURA ZA MAONI KESHO

HANDENI MJINI KURUDIA KURA ZA MAONI KESHO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo, Novemba 02,2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili kwa kina mapendekezo ya wana CCM walioomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo la Handeni mjini.

 Kamati Kuu imetengua mapendekezo ya awali na kuagiza kurejewa kwa mchakato wa kura za maoni kwa wana -CCM wawili walioongoza kura za maoni za awali.

Wana- CCM hao watakaopigiwa kura za maoni tena kesho Novemba 03,2015 ni pamoja na Omari Abdallah Kigoda na Hamis Hamad Mnondwa.

Aidha Kamati Kuu imeteua wajumbe watatu kusimamia zoezi hilo ambao ni Dk. Maua Daftari, Dk.Emmanuel Nchimbi na Alhaji Abdallah Bulembo.


0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa