Home » » MABASI YAPATA AJALI TANGA NA MOROGORO NA KUUWA WATU KADHAA HII LEO

MABASI YAPATA AJALI TANGA NA MOROGORO NA KUUWA WATU KADHAA HII LEO


Basi la Ngorika lililokuwa kitoka jijini Dar es Salaam kwenda Arusha  na lile la Kampuni ya RATCO Tanga kwenda Dar es Salaam yamegongana uso kwa huso na kulihusisha gari lingine dogo aina ya Noah na kusababisha vifo vya abiria na majeruhi.Ajali hiyo ilitokea eneo la Mbweni Mkata mkoni Tanga. 

Wakati huo huo habari kutoka Morogoro zinaarifu kuwa Basi mali ya kampuni ya Happy Nation lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mbeya limepata ajali eneo la Kikwaraza Mikumi na kuuwa watu wawili na kusababisha majeraha kwa abiria wengine 48.
 Basi la Ngorika likiwa limeharibika vibaya.
Gari dogo aina ya Noah lililohusika katika ajali ya Tanga na abiria wake wote waliokuwa wa fami;lia moja kuripotiwa kufa.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa