Home » » JESHI LA POLISI NCHINI LIMEONGEZA ASKARI WA VIKOSI VYA ARDHINI KUKABILIANA NA VIKUNDI VYA KIGAIDI MKOANI TANGA.

JESHI LA POLISI NCHINI LIMEONGEZA ASKARI WA VIKOSI VYA ARDHINI KUKABILIANA NA VIKUNDI VYA KIGAIDI MKOANI TANGA.

 
Jeshi la wananchi kwa kushirikiana na polisi nchini limeongeza askari wa vikosi vya ardhini katika zoezi la kukabiliana na vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi katika mapango ya mleni yaliyopo eneo la amboni jijini Tanga kufuatia askari wa jeshi la wananchi kuuawa kwa risasi huku wengine wakijeruhiwa katika mapigano baina yao na vikundi hivyo.
ITV imeshuhudia msafara wa magari ya kijeshi pamoja na yale ya maofisa wa kijeshi na huduma ya kwanza yakipita katika barabara kuu itokayo Tanga kwenda Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kisha kuingia katika njia iendayo katika mapango yaliyodaiwa kuwa ni sehemu maalum ya maficho ya vikundi hivyo vya kigaidi na msemaji wa polisi kamishna wa polisi -operesheni Paul Chagonja kutwa nzima simu yake iliita bila majibu lakini msaidizi wake alipoke na kudai kuwa bosi wake yupo kwenye kikao.
 
Hata hivyo baadhi ya familia zilizopo katika eneo la mleni zinadaiwa kuhamisha makazi kufuatia milipuko ya risasi na silaha nzito za kijeshi zilizokuwa zikirindima katika kipindi cha siku mbili nyakati za mchana na usiku hatua ambayo baadhi ya makundi ya vijana yanaojihusisha na kazi ya kupasua mawe katika mapango hayo kulalamikia ukosefu wa kazi kwa sababu ya mapigano hayo ambayo pia yamewapa hofu na maisha yao.
 
Baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameshauri mapango hayo yaharibiwe kwa kutumia vifaa maalum vya kivita na jeshi la polisi lisahau suala la silaha zao zilizoibwa katika matukio tofauti na makundi hayo.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa