Home » » ‘TUFADHINI MAJI YA MVUA YATUSAIDIE KIANGAZI’

‘TUFADHINI MAJI YA MVUA YATUSAIDIE KIANGAZI’

Wakulima wa mbogamboga na matunda wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga wametakiwa kuzitumia mvua zinazonyesha kuhifadhi maji ili yawasaidie wakati wa kiangazi.
Mkurugenzi wa Muungano wa Wakulima Vijijini (Yadet), Maira Rebule alisema hayo jana na kuongeza kuwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi, wilaya hiyo huwa inakosa mvua mara kwa mara.
“Nadhani tumekutana muda muafaka wa kujadili na kujiwekea mikakati ya kilimo chetu cha mbogamboga na matunda, ambacho kwa kiasi kimepoteza dira, kila mtu anatambua kuwa Lushoto ndiyo kitovu cha matunda.

“Kwa vile mvua zimeanza kunyesha ni wajibu wetu kuanza kulima na kujiwekea utaratibu wa kuhifadhi maji hayo kwa kuyatega ili yatusaidie baada ya msimu wa mvua kumalizika,” alisema Rebule katika kongamano la wakulima hao.
Mkulima wa kabichi na njegere, Abrahman Shedafa alizitaka kampuni na taasisi za watu binafsi kujenga kiwanda cha kusindika matunda ili wawe na uhakika wa soko.
Alisema wakati wa mavuno wakulima wengi huwa wanauza matunda na mbogamboga kwa bei ya hasara ili kuepuka mazao kuharibika kutokana na kukosa soko.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukilalamika upatikanaji wa soko la kuuzia matunda na mbogamboga...kipindi cha mavuno tunakuwa katika wakati mgumu na kushindwa kujua la kufanya,” alisema Shedafa.
Alisema kama Serikali itaweka msukumo wa kujenga kiwanda cha kusindika matunda, wakulima wengi watafaidika.
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa