Home » » BREAKING NEWS: BASI LA DAR EXPRESS LAKAMATWA NA SHEHENA YA MIRUNGI KITUO CHA CHEKERI KOROGWE LIKITOKEA ARUSHA

BREAKING NEWS: BASI LA DAR EXPRESS LAKAMATWA NA SHEHENA YA MIRUNGI KITUO CHA CHEKERI KOROGWE LIKITOKEA ARUSHA

 Taarifa zilizotufikia muda huu ambazo Hazijathibitishwa Rasmi zinasema kwamba Basi la Dar Express lenye namba za usajili T 244 BXQ limekamatwa na Gunia zaidi ya 16 za Mirungi katika kituo cha ukaguzi cha Chekeri Korogwe Likitokea Arusha Basi Hilo lilikamatwa Jana Majira ya Saa nane Mchana na kupelekwa mpaka katika kituo cha wilaya cha Polisi Korogwe, mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhisiwa anahusika na tukio hilo pia Konda wa Basi hilo anashikiriwa na Polisi. Endelea kufuatilia hapa Taarifa kamili inakuja mapema leo.
 Basi la Dar Express likiwa limesimamishwa kwa ajili ya Ukaguzi huo
 Ukaguzi wa Basi hilo ukiwa unaendelea

 Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa wanapakia Magunia ya Mirungi katika Gari lao


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa