Home » » WAZAZI TANGA WAPEWA USHAURI

WAZAZI TANGA WAPEWA USHAURI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WAZAZI wametakiwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni ikiwa ni pamoja na kushirikiana na walimu ili kuweza kuthibiti utoro.
Akizungumza juzi wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Haki na Ulinzi wa Mtoto kwa klabu za wanafunzi shuleni kilichochapishwa na Shirika la Passadit, Katibu Tawala Wilaya ya Tanga, Bernard Marselline, alisema Mkoa huo unakabiliwa na tatizo la utoro hatua inayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu.
Marselline, alisema kuna aliwataka walimu kuhakikisha wanatoa taarifa juu ya vitendo vya utoro na mimba shuleni na iwapo watashindwa kuripoti matukio hayo hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa walimu hao.
Katibu huyo aliwakemea wazazi hao kuacha kuwaoza mabinti zao wakati wakiwa shuleni na badala yake kusimamia kwa ukaribu maendeleo yao ili wafanye vema katika masomo yao.
Naye Mratibu wa Shirika la Passadit, Simon Stephano, alisema shirika lake kwa miaka mingi limekuwa likifanya utafiti mitaani na kubaini ukatili wa kijinsia kwa watoto ukiendelea.
Alisema wamechapa kitabu hicho ili kuwawezesha jamii ya watoto kuelewa haki zao hivyo kitabu hicho kitatoa muongozo hatua itakayosaidia kutokomeza vitendo vya unyanyasaji vinavyofanyika katika jamii.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa