Home » » POLISI WAZUIA MKUTANO CHADEMA, WARUHUSU CCM

POLISI WAZUIA MKUTANO CHADEMA, WARUHUSU CCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa MomboBAADHI ya wananchi wa Mji wa Mombo wamedai, hawajafurahishwa na Jeshi la Polisi mjini hapa, kuzuia mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kuruhusu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa wananchi hao, walidai kuwa Polisi jana ilizuia kutoa kibali kwa CHADEMA iliyoomba kufanya Mkutano katika Mji Mdogo wa Mombo Ijumaa ijayo kisha kuruhusu CCM ifanye mkutano katika mji huo.
Polisi mmoja ambaye hakutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, alikiri kuwa chadema wamenyimwa kibali kwa kuwa wameomba maandamano na mkutano.
“CHADEMA walizuiwa kwa sababu waliomba Kibali cha Maandamano na Mkutano, hivyo kwa kuwa maandamano yamepigwa Marufuku nchi yote, hawakuruhusiwa kufanya hivyo na kwamba kitendo cha kufanya hivyo bila kibali, watalazimika kuwatawanya.
“Ni kweli CCM wamekubaliwa kufanya Mkutano hapa Mombo Ijumaa, Septemba 26, utakaohutubiwa na Kinana, na CHADEMA tuliwaruhusu kama wanataka kufanya Mkutano wafanye Mombo, Septemba 26, lakini si Maandamano”, alisema.
Mwenyekiti wa CHADEMA Korogwe, Aurelian Nziku, alisema kuwa waliomba kibali cha kufanya maandamano ya amani na mkutano ila polisi imezuia maandamano na kuruhusu mkutano wa CCM, ila wao pia wameruhusiwa kufanya mkutano mwishoni mwa wiki.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa