Home » » MOTO WATEKETEZA MADUKA TANGA

MOTO WATEKETEZA MADUKA TANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MADUKA manne yameteketea kwa moto kutokana na hitilafu ya umeme barabara ya 14 jirani na stendi ya mabasi yaendayo mikoani jijini Tanga, usiku wa kuamkia jana.
Moto huo uliozuka majira ya saa tatu na nusu usiku katika eneo hilo, inaelezwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyosababishwa na kutokuzimwa kwa baadhi ya vifaa.
Bakari Shabani ambaye ni shuhuda wa tukio hilo, alisema alishangaa kuona moshi ukitoka juu ya mlango wa duka moja linalouza vifaa vya umeme ndipo alipowaambia wenzake ili kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto.
“Mimi nilikuwa katika biashara yangu ya chipsi jirani kabisa na maduka haya, mara ghafla nikashangaa kuona moshi ukitokea kwa juu… si ndipo nilipopiga kelele ili watu waje,” alisema Shabani.
Alisema kuwa Zimamoto walifika katika tukio na kuanza taratibu za uokoaji ingawaje hawakufanikiwa kwa kiasi kikubwa, kwani tayari vitu vilivyokuwemo vilikuwa vimeshateketea.
Akizungumza na Tanzania Daima, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga, Charo Mangare, alisema kuwa ni vema wafanyabiashara kufunga mitungi ya kuzimia moto ‘Fire extinguisher’ ili kutatua matatizo ambayo yanaweza kutokea katika majanga hayo ya moto.
Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo unaendelea
Chanzo; Tanzania Daima 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa