Home » » TANESCO KUWABANA WAWEKEZAJI WABABAISHAJI

TANESCO KUWABANA WAWEKEZAJI WABABAISHAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WIZARA ya Nishati na Madini imesema itahakikisha haitoi mwanya kwa wawezezaji wababaishaji wanaotaka kuwekeza kwenye nishati ya umeme na kuwaingiza Watanzania kwenye mgawo wa umeme bila sababu.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi, alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama cha wafanyakazi, TUICO matawi ya Shirika la Umeme (Tanesco) na viongozi wa wizara.
Alisema asilimia 24 ya Watanzania zaidi ya milion 44 ndio waliounganishwa na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali vijijini na mijini.
Maswi alisema kiwango hicho kinaonyesha kwamba kuna watanzania wengi wanaotumia mkaa na kuharibu mazingira nchini.
Kwa sababu hiyo idadi serikali kupitia sekta ndogo ya nishati ya umeme inadhaniria kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felichesmi Mramba, alisema shirika hilo limeanza kufanya vizuri huku akisema ifikapo mwaka 2033 asilimia 75 ya Watanzania watanufaika na huduma hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, alisema mkoa huo umedhamiria kuinua pato la mtu mmoja mmoja, hivyo anaamini kwamba kupitia umeme Watanzania wengi watanufaika na huduma bora za shirika hilo
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa