Home » » SERKALI YASAKA WAFADHILI KUJENGA KIWANDA MKINGA

SERKALI YASAKA WAFADHILI KUJENGA KIWANDA MKINGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
SERIKALI inaandaa mpango wa kuomba wafadhili wa ndani na nje ya nchi utakaowawezesha kujengea kiwanda cha kubangulia korosho kwa wakulima wa zao hilo walayani Mkinga, Tanga.
Ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kumaliza tatizo la wakulima wa korosho katika wilaya hiyo wanaouza zao hilo kwa walanguzi wa nchi za jirani.
Akifungua semina ya siku tatu ya wakufunzi na wanafunzi wa mafunzo ya korosho yaliyofanyika Maramba wilayani Mkinga, Mkuu wa Wilaya hiyo Mboni Mgaza alisema uuzaji wa korosho kwa walanguzi ni changamoto kwa wakulima.
Aliwaambia  wadau wa semina hiyo iliyoandaliwa na Kituo cha Utafiti wa korosho cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara kwamba kuvushwa kwa zao hilo kwenda Kenya kunawafanya wakulima wapate bei ndogo kutoka kwa walanguzi.
“Si hivyo tu athari nyingine ni upotevu wa mapato ya ushuru ambayo yangepatikana iwapo korosho ingeuzwa katika soko rasmi na kuliingiza pato taifa,” alisema Mgaza.
Mgaza alivitaka vijiji vya Mkinga leo, Mwanyumba, Horohoro na Kwangena ambao ni wakulima wa korosho kuwa chachu ya kukataa kuuza zao hilo kwa bei ndogo kwa walanguzi kitendo kinachodidimiza
vipato vyao.
Naye Dk. Louis Kasuga kutoka Chuo cha Utafiti cha Naliendele, alisema mafunzo hayo yanalenga kuwakumbusha wadau kuboresha na kuyatunza mashamba yao.
‘’Tunawahamasisha wapande mbegu bora zenye sifa zinazotakiwa ili kupata mazao bora ya kutosha… wadau pia wafufue mikorosho iliyotelekezwa,” alisema Dk. Kasuga.
Wilaya ya Mkinga inao wakulima 2,565 waliopo sasa tofauti na wakulima 1,089 waliokuwepo hadi mwishoni mwa mwaka jana, hali hiyo ni sawa na ongezeko la wakulima 1,476.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa