Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Kibirashi, wilayani Kilindi,
Yussuph Mwegango na viongozi wenzake wanne wa ngazi ya vitongoji,
vijiji, kata na tarafa wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kushawishi
mapigano kati ya wakulima na wafugaji ambayo yalisababisha vifo vya
watu wawili.
Wiki iliyopita watu wanane walijeruhiwa vibaya huku wawili kati yao
wakipigwa risasi na polisi kutokana na mapigano ya kugombea ardhi
wilayani Kilindi.
Mapigano hayo yalisababisha wakulima kuteka Kijiji cha Kiberashi kwa
kutumia silaha baridi kisha kuvunja nyumba mbili za kisasa, kuteketeza
pikipiki nne na baadaye kupora mali katika maduka ya wafanyabiashara wa
jamii ya wafugaji.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi,
Selemani Liwowa, aliwataja viongozi wengine kuwa ni Salim Rajab
(Mwenyekiti Kitongoji cha Kibirashi), Ayoub Hajji (Mjumbe wa Serikli ya
Kijiji cha Kibirashi) na Zubeir Machaku (Ofisa Mtendaji Kijiji cha
Kibirashi).
“Kwa sasa hali ni shwari kutokana na kuongeza nguvu za kiusalama
kwani askari kutoka wilaya za Kilindi, Handeni na Tanga wameweka kambi
maalumu ya ulinzi katika kijiji hicho ili kuhakikisha hali inarudi
kuwa ya usalama,” alisema.
kuwa ya usalama,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment