Home » » PONGWE WALILIA GARI LA WAGONJWA

PONGWE WALILIA GARI LA WAGONJWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
UKOSEFU wa gari la wagonjwa katika kituo cha afya Pongwe kilichopo kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga unasababisha mazingira magumu ya kuwasafirisha wagonjwa wanaohitaji huduma zaidi za kimatibabu kutoka maeneo ya mbali na kituo hicho.
Akizungumza katika hafla fupi ya wafanyakazi kujipongeza kwa  mafanikio waliyopata kwa utoaji wa huduma bora zikiwemo za wajawazito na watoto jana, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Faisal Ali, alisema wamepokea wagonjwa kutoka vijiji mbalimbali na baadhi yao kuwa na kesi za kupata tiba hospitali nyingine, hivyo huwa vigumu kuwasafirisha.
“Hiki kituo unaweza kukiona ni kidogo ila kiutendaji ni kikubwa, hakuna mtu ambaye hajui kama tunahudumia mamia ya watu kwa siku, tatizo ni pale mgonjwa au mjamzito tunapotaka kumpeleka Hospitali ya Bombo ndiyo balaa, hatuna gari,” alisema Dk. Ali.
Aliiomba serikali kupeleka gari la wagonjwa katika kituo hicho ili kukabiliana na changamoto za wajawazito wakati wa kujifungua na utoaji wa elimu ya umuhimu wa kuhudhuria kiliniki.
Kwa mujibu wa Dk. Ali, baadhi ya wanawake hasa wa vijijini hawajui umuhimu wa kuhudhuria kliniki ili kujua mwenendo wa ujauzito.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Msaidizi Afya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Yombo Shelufumo, aliwataka wafanyakazi hao kutobweteka na mafaniko waliyoyapata na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii ili kuyafikia mafanikio zaidi.
Alisema mbali ya changamoto nyingi wanazokabiliana nazo, zikiwemo za kupandishwa vyeo na umbali wa wafanyakazi wanapoishi, serikali inatambua na hivyo kuwataka kufanya kazi kwa bidii.
Shelufumo alisema siri ya mafaniko ni kufanya kazi kwa bidii, na hivyo kuwataka kufanya uvumilivu huku serikali ikitambua changamoto hizo na kuzifanyia kazi zikiwemo za kuwapandisha vyeo.
Chanzo;anzania Daima 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa